Home KITAIFA DUH…ALICHOSEMA MPOLE MMEKISIKIA AISEE…ADAI MAMBO NI MAGUMU KWA GEITA…

DUH…ALICHOSEMA MPOLE MMEKISIKIA AISEE…ADAI MAMBO NI MAGUMU KWA GEITA…

0

 

Mfungaji Bora msimu uliopita, George Mpole aliyemaliza Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 17, amesema ameshindwa kufunga kwenye mechi mbili mfululizo za awali za ligi hiyo kutokana na kukamiwa sana na mabeki, lakini akitamba amejipanga kuwapa raha mashabiki ligi itakaporejea baada ya mapumziko.

Ligi imesimama baada ya kuchezwa mechi 16 za raundi mbili, huku Mpole akiwa hana bao ilhali washindani wake msimu uliopita, Reliants Lusajo wa Namungo na Fiston Mayele wakitupia katika mechi zote na kuanzisha vita mpya msimu huu.

Mpole alisema Geita ilianza ligi na ratiba ngumu kwa kucheza mechi mbili ugenini tena dhidi ya Simba na Azam, hivyo haikuwa kazi ndogo kwao, licha ya kuambulia pointi moja tu hadi sasa..

“Kazi yangu ni kufunga mabao ili kuisaidia timu na nilitaka iwe hivyo ila nilikutana na zaidi ya ugumu kutoka kwa mabeki wa timu hizo mbili pengine tofauti na nilivyokutana nao msimu uliopita..naamini uwezo wangu na nitafunga mabao,” alisema Mpole.

THIS POST IS POSTED IN SOKA LEO AND APPEAR IN THIS APP

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here