Klabu ya Manchester United imeingilia dili la usajili wa Pierre Emerick Aubameyang anayetarajiwa kutimkia Chelsea kuungana na kocha wake wa zamani Thomas Tuchel.
Tayari mazungumzo kati ya klabu ya Chelsea na mchezaji yameshafanyika ikiwa ni pamoja na kukubaliana maslahi binafsi inagawa kikwazo kimebaki kati ya vilabu vyote viwili kukubaliana ada ya uhamisho.
Klabu ya Barcelona ambao nddiyo wamiliki wa mchezaji huyo wamebainisha kuhitaji kiasi cha Euro milioni 25 huku Chelsea wao wakiwa tayari kutoa Euro milioni 15 tu.
Kutokana na hali hiyo Manchester United wameingilia dili kati na kutaka kumaliza biashara mapema na klabu ya Barcelona ili kuinasa Saini ya Aubameyang.
Aubameyang (33) alisajiliwa na Barcelona majira ya baridi akitokea klabu ya Arsenal lakini kutokana na ingizo la mshambuliaji raia wa Poland Robert Lewandowski ndani ya Nou Camp nafasi ya Aubameyang kuanza imeonekana kuwa ndogo na hivyo kumlazimu kutafutana nafasi katika timu nyingine ambapo ataenda kuwa chaguo la kwanza.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE