Home KITAIFA YANGA KUIKABILI AZAM KWA MBINU TOFAUTI

YANGA KUIKABILI AZAM KWA MBINU TOFAUTI

0

 

Nesreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amebainisha kuwa atabadili mbinu kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC.

Kocha huyo amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili na kushinda zote ugenini.

IlikuwaPolisi Tanzania 1-2 Yanga na Coastal Union 0-2 Yanga zote zilichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mchezo ujao utakuwa ni wa kwanza kwa Nabi kuingoza timu hiyo kwa msimu wa 2022/23 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Nabi amesema:”Ni mchezo muhimu kwetu kupata matokeo zile mbinu ambazo tulizitumia kwenye mechi zetu ugenini lazima zitabadilika kwani kila mchezo unahitaji mpango kazi tofauti.

“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuwa tayari kwenye mchezo wetu ujao na tunaamini kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari,” amesema.

 Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 6,2022.

THIS POST IS POSTED IN SOKA LEO AND APPEAR IN THIS APP

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here