Home KITAIFA AHMED ALLY: TULIACHANA NA ZARON SABABU ALIKATAA BAADHI YA WACHEZAJI WETU

AHMED ALLY: TULIACHANA NA ZARON SABABU ALIKATAA BAADHI YA WACHEZAJI WETU

0

Msemaji wa Simba Ahmed Ally amesema miongoni mwa sababu ambazo ziliwafanya wasikie hatua ya kuachana na aliyekuwa Kocha wao Mkuu Zoran Maki ni kuwakataa baadhi ya wachezaji.

Ahmed ameyasema hayo Septemba 16, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV akielezea maandalizi yao ya mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi ambapo alipoulizwa kuhusu sababu ya kuachana na Zoran ndipo aliposema sababu hiyo.

“Hiyo ya kuwakataa baadhi ya wachezaji ni miongoni mwa sababu ambayo ilitufanya tuachane na Zoran lakini kwa ujumla tulifikia mahali tukaona hatuwezi kwenda pamoja na Zoran, na yeye akaona hawezi kufanya kazi na Simba,” alisema Ahmed.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here