Home KITAIFA ALICHOKISEMA MWAKINYO BAADA YA TAARIFA ZA KUFUNGIWA UINGEREZA KUSAMBAA

ALICHOKISEMA MWAKINYO BAADA YA TAARIFA ZA KUFUNGIWA UINGEREZA KUSAMBAA

0

Bondia wa Kimataifa kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo ametolea maelezo kuhusu taarifa za kufungiwa kucheza pambano lolote nchini Uingereza mpaka pale ambapo taarifa nyingine itatolewa.

Mwakinyo alipoteza pambano lake la mwisho la raundi 12 kwa TKO Majuma kadhaa yaliyopita nchini humo baada ya kupigwa na Liam Smith katika raundi ya nne tu huku yeye akidai kuwa alifanyiwa figisu na kuoewa viatu vya kubana vilivyomsababishia matatizo wakati akipigana.

Mwakinyo, ameandika; “Punguzeni mihemko, guys naomba niweke sawa kuhusiana na huo uvumi mimi sijafungiwa kama wanahabari wanavyoeneza ila “British Boxing Border Control” ni moja ya sheria yake hairuhusu mchezaji yoyote aliepoteza kwa TKO au KO kurudi ulingoni kwa muda wa siku 45 zipite mpaka siku 60.

“Llakini hio haimaanishi mtu huyo kuvunja sheria au kufanya kosa lolote lile ambalo litagharimu yeye kutocheza pale tena.

“Nimeweka picha mbili hapo uki swipe utanielewa na muwe makini na habari hizo mnazoeneza. Ukiwa mwana habari wa michezo lazima ujifunze kujua sheria kabla kuongelea jambo,” amesema Mwakinyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here