Home KIMATAIFA BAADA YA KUFUKUZWA KWA JEURI AL AHLY YA MISRI…PITSO MOSIMANE ALAMBA SHAVU...

BAADA YA KUFUKUZWA KWA JEURI AL AHLY YA MISRI…PITSO MOSIMANE ALAMBA SHAVU SAUDIA

0

Klabu ya Al Ahli Jedda imemtangaza Kocha Mosimane raia wa Afrika Kusini kuwa kocha wao Mkuu asubuhi ya leo Jumapili, Septemba 25, 2022 akichukua nafasi ya kocha Yousef Anbar.
Al Ahli Saudi Fc ilishuka daraja msimu uliopita na Sasa inashiriki ligi daraja la pili nchini Saudi Arabia.

“Pitso Mosimane ni kocha mpya wa timu yetu ya soka,” imesema sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.

Taarifa zinasema kuwa , Pitso atakuwa akilipwa zaidi ya Milioni 600 kwa mwaka kama sehemu ya mshahara wake nnje ya marupurupu na bonasi za ushindi.

Pitso ni kocha namba moja Afrika ambaye amepata mafanikio makubwa akiwa Mamelodi Sundowns ya nchini kwao kisha Al Ahly ya Misri ambayo aliachana nayo miezi michache iliyopita.

Pitso ambaye alijiunga na Ahly mwaka 2020 amefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa Afrika mara tatu ndani ya miezi 21 aliyowatumikia Mafarao hao wa Misri na kushinda fainali mbili kati ya hizo mfululizo.

Amefanikiwa kushika nafasi ya tatu mara mbili mfululizo katika kombe la Fifa la Vilabu Bingwa Duniani, CAF Super Cup mbili, ubingwa wa Misri mara mbili na makombe kadhaa ya Misri.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here