Home KITAIFA BAADA YA KUKOSA NAFASI YA KUCHEZA, AKPAN AVUNJA UKIMNYA SIMBA

BAADA YA KUKOSA NAFASI YA KUCHEZA, AKPAN AVUNJA UKIMNYA SIMBA

0

Ukimya na kutoonekana kwa Kiungo Kutoka nchini Nigeria Victor Patrick Akpan, umemuibua hadharani Mchezaji huyo na kuwajibu Mashabiki na Wanachama wa Simba SC walioingia wasiwasi dhidi yake.

Kwa kipindi cha majuma mawili Akpan amekua haonekani sambamba na wachezaji wenzake wa Simba SC, hali ambayo imezua taharuki kwa Mashabiki na Wanachama wa Msimbazi.

Kiungo huyo aliyesajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu huu 2022/23 akitokea Coastal Union ya jijini Tanga, amesema bado ni mchezaji halali wa Simba SC na hajaachwa kama baadhi ya Mashabiki na Wanachama wanavyodhani.

“Niwatoe hofu Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, mimi bado ni mchezaji halali wa Simba SC, nipo na nitaendelea kuwepo kwa mujibu wa mkataba wangu wa miaka miwili.”

“Ni kweli sijaonekana kwa siku kadhaa nikiwa sambamba na wachezaji wenzangu, hii imetokana na majereha ya goti yanayonikabili kwa sasa, lakini namshukuru Mungu ninaendelea vizuri, muda si mrefu nitaanza mazoezi mepesi.”

“Mashabiki na Wanachama waendelee kuniombea na kuiombea timu yetu ili kufanikisha tunachokikusudia msimu huu, lengo kubwa ni kufanya vizuri na kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara pamoja na kuvuka hatua ya Robo Fainali Kimataifa.” amesema Akpan

Mara ya Mwisho Akpan alionekana akiwa sambamba na Wachezaji wenzake wa Simba SC wakati wa Michezo ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, Al Hilal ya Sudan na Arta Solar ya Djibout mwishoni mwa mwezi uliopita.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here