Home KIMATAIFA BAADA YA KUSIKIA WAANGOLA WANAFUJO WAKICHEZA KWAO…SIMBA NAO WAANZA KUWATISHA MAPEMA

BAADA YA KUSIKIA WAANGOLA WANAFUJO WAKICHEZA KWAO…SIMBA NAO WAANZA KUWATISHA MAPEMA

0

Uongozi wa Klabu wa Simba umewaambia wapinzani wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Clube Desportivo 1º de Agosto ya nchini Angola kuwa kamwe hawatakubali kufanyiwa vitendo vya kihuni kuanzia ndani hadi nje ya uwanja na wao wakakaa kimya, ni lazima watajibu mapigo.

Kauli hiyo imetolewa wakati Simba ikijiandaa kwenda kuvaana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo ambao utapigwa kati ya Oktoba 7-9, mwaka huu huko nchini Angola.

Simba itavaana dhidi ya Agosto baada ya kufanikiwa kuwaondoa Nyasa Big Bullets kwa ushindi wa jumla mabao 4-0.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa uongozi unafahamu uhuni wote wanaoufanya Clube Desportivo 1º de Agosto wakiwa nyumbani kwao, hivyo wamejiandaa kupambana nao.

Ally alisema kuwa kamwe hawatavumilia vitendo vya kihuni watakavyovifanya wapinzani wao wakiwa nyumbani kwao, badala yake watalipiza huko ugenini kabla ya kurudiana hapa nyumbani.

Aliongeza kuwa, uongozi umejipanga katika kila kitu kitakachotokea ugenini baada ya kuanza maandalizi ya kuhakikisha wanapambana na kila hujuma itakayotokea.

“Tumepanga kuwahi mapema Angola kwa maana ya viongozi kuandaa mazingira mazuri itakayofikia timu kwa maana ya hoteli, uwanja wa kufanyia mazoezi pamoja na chakula.

“Hiyo ni baada ya kuujua uhuni wote kwa maana ya hujuma wanazotumia, kama uongozi tumejiandaa na kila uhuni watakaoufanya wa ndani na nje ya uwanja.

“Hivyo wakae wakijua kwamba hatutavumilia kwa kila uhuni watakaoufanya mara baada ya kuingia katika ardhi ya Angola, tena wasijaribu kabisa kingine wafahamu kabisa lazima na wao waje hapa nchini,” alisema Ally.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here