Home KITAIFA CLATOUS CHAMA KUWAHI DODOMA JUMAPILI

CLATOUS CHAMA KUWAHI DODOMA JUMAPILI

0

CLATOUS Chama nyota wa kikosi cha Simba raia wa Zambia anatarajiwa kuwa miongoni mwa watakaokuwa kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Jumapili.

Chama ambaye yupo kwenye fainali ya kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi ndani ya Simba chaguo la mashabiki hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoweka kambi Zanzibar.

Sababu kubwa ya kukosekana kwake ni matatizo ya kifamilia ambayo kwa sasa tayari kila kitu kimeweza kwenda sawa.

Kikosi cha Simba kimerejea Dar baada ya kucheza mechi mbiliza kirafiki ilikuwa Malindi 0-1 Simba na Kipanga 0-3 Simba, mchezo wao ujao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili.

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na mechi za kimataifa.

“Mechi ambazo tumecheza za kirafiki hizo ni nzuri kwetu na zimezidi kutuimarisha hivyo tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu zijazo kitaifa na kimataifa na wachezaji wapo tayari,” .

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here