Home KITAIFA HIVI NDIVO BODI YA LIGI WANAVYOZIPUNA SIMBA NA YANGA MAMILIONI YA PESA...

HIVI NDIVO BODI YA LIGI WANAVYOZIPUNA SIMBA NA YANGA MAMILIONI YA PESA KIULAAINI KABISA

0

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu imeingizia Bodi ya Ligi (TPLB) Sh17.8 milioni kupitia matukio mbalimbali waliyoyatolea uamuzi katika raundi nne za kwanza msimu huu.

Bodi ilianza kupata fedha kwenye mchezo wa Polisi Tanzania na Yanga, baada ya mashabiki wa Yanga kurusha chupa za maji uwanjani na mabingwa watetezi kutozwa faini ya Sh1 milioni.

Coastal Union nayo ilitozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la baadhi ya maofisa wake kumwaga vitu vyenye asili ya kimiminika uwanjani wakati wakipasha misuli moto kwenye mchezo wao dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Upande wa Kagera Sugar nayo ilitozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la baadhi ya wachezaji na maofisa wake kumwaga vitu vyenye asili ya mbegu katika mchezo wao dhidi ya Azam FC uliochezwa kwenye Azam Complex.

Kamati iliendelea kuiingiza bodi baada ya kuona tukio lengine kwenye mchezo wa Polisi Tanzania na KMC, Polisi ikitozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la wachezaji wake kumwaga vitu vyenye asili ya unga, wakati wakiingia uwanjani kupasha misuli moto kabla ya mchezo, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Yanga ilitozwa tena faini ya Sh500,000 kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union kwa kosa la kufanya mabadiliko ya wachezaji kwa mikupuo minne badala ya mitatu, mchezo uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Kagera Sugar ikatozwa faini Sh500,000 kwa kosa la kugoma kutumia chumba rasmi cha kuvalia kabla na wakati wa mapumziko kwenye mchezo wao na Simba katika Uwanja wa Mkapa.

Wakati huo huo, kamati ilizitoza Kagera Sugar na Dodoma Jiji faini ya Sh3 milioni kwa kila mmoja kwa kosa la kushindwa kuvaa jezi ya mdhamini mkuu. Kagera ilitenda kosa hilo katika mchezo dhidi ya Simba na Dodoma Jiji dhidi ya Tanzania Prisons.

Rungu likaishukia tena Dodoma Jiji kwa kupigwa faini ya Sh3 milioni kwa kosa la kushindwa kuweka mabango ya wadhamini wake binafsi kwenye Uwanja wa Liti, Singida wakati ilipocheza na Tanzania Prisons.

Kamati hiyo ilikuja kupitia tena mwenendo wa Ligi na kukuta makosa kwenye mchezo wa Geita Gold dhidi ya Kagera Sugar na kuzipiga faini Sh1 milioni kila mmoja kwa kosa la kuchelewa kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Yanga imeingia kwa mara nyingine kwenye adhabu lakini safari hii ni kwa mchezaji wake, Bernard Morrison akifungiwa mechi tatu na kutozwa faini Sh1 milioni kwa kosa la kumkanyaga makusudi Lusajo Mwaikenda.

Ruvu Shooting ilipigwa faini ya Sh3 milioni kwa kosa la kushindwa kuweka mabango ya wadhamini wake binafsi kwenye uUwanja wa Uhuru, wakati wa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.

Kamati ilimalizia kwa mchezaji wa Dodoma Jiji, Rajab Habibi akifungiwa mechi tatu na kutozwa faini Sh500,000 kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here