Home KITAIFA ISHU YA DEJAN KUVUNJA MKATABA MSIMBAZI…SHAFII DAUDA AIBUKA NA HILI JIPYA

ISHU YA DEJAN KUVUNJA MKATABA MSIMBAZI…SHAFII DAUDA AIBUKA NA HILI JIPYA

0

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka, Shaffih Dauda amedai kuwa kuna tatizo ndani ya Klabu ya Simba hali inayopelekea mambo yao kutokwenda sawa na kupishana baadhi ya mambo.

Kauli hiyo ya Dauda inakuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Simba kuachana na mshambuliaji wao, Dejan Georgijevic raia wa Serbia.

“Mimi niliwaambia kuwa kuna vitu havipo sawa ndani ya Simba, ni juzi tu nilitoka kuwaambia hapa hapa mkaona nawakebehi, mkahisi siwatakii mema na kuamini nina agenda binafsi.

“DIGALA sipo hapa kuonea mtu wala timu, sipo hapa kusema uongo ili kiwe nini? Huko tushapita, kila nikitaka niwape dawa naona mnakimbia drip kwa kuamini panadol inatosha kupooza maumivu.

“Jana pia nimetoka kuwaambia mkishaenea darasani mwambieni Kiranja aje kuniita niwape darasa zuri sana Simba ila mkakaidi, kwasasa nawapa muda mjitafakari kisha DIGALA nitazungumza kuwaambia wapi mnakosea huko ndani.

“Kubalini drip la DIGALA liwaingie, ni dawa nzuri sana kuliko hizo panadol zenu mnazopeana kuwa nawachukia, nawapenda sana, nataka niwaweke sawa.

“Nasubiri Press Release nipo pale nimekaa, mkienea darasani basi mtumeni Kiranja aje kuniita. THIS IS DIGALA.” ameandika Shaffih kupitia ukurasa wake wa Instagram.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here