Ikiwa zimepita siku chache tangu Ally Kamwe atangazwe kuwa Afisa Habari wa Klabu Kongwe nchini Yanga Afrika.
Kumeibuka minong’ono kuwa amekwenda kuchukua nafasi ya aliekuwa msemaji wa Yanga ambae kwa sasa anatumikia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa miaka miwili Haji Manara.
Sasa jana Septemba 29, akizungumza kupitia kipindi cha michezo cha Sports Arena kinachorushwa na Wasafi FM, Ally Kamwe amekanusha uzushi huo huku akiweka wazi haji bado yuko Yanga na wanafanya kazi pamoja.
“Labda leo niwaweke wazi ili watu wote wanaozungumza waweze kufahamu, Mimi ni Afisa Habari wa Yanga, Haji ni Msemaji rasmi wa Klabu na hatuingiliani katika majukumu”
“Haji mpaka leo ni mfanyakazi wa Yanga ambae amefungiwa hivyo anashindwa kutimiza baadhi ya majukumu lakini kazini anafika”
“Mbona Bumbuli na Nugaz walikuwa pamoja na watu hawakuleta haya maneno” amesisitiza Ally.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE