Home KITAIFA KISA UWEPO WA KISINDA, MAKAMBO AWASHIWA TAA NYEKUNDU YANGA

KISA UWEPO WA KISINDA, MAKAMBO AWASHIWA TAA NYEKUNDU YANGA

0

Ujio wa Tuisila Kisinda ndani ya Yanga baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF kutoa baraka zake kuanza kuitumikia timu hiyo, imewasha taa ya tahadhari kwa mshambuliaji Heritier Makambo kuendelea kusalia katika kikosi hicho, ili naye ampishe nyota mwingine aliyepo nje kwa sasa.

Za Ndaani Kabisa kutoka Yanga zinasema, Makambo anapaswa kuwasha moto ili dirisha dogo limpite salama, kwani mipango ni kumrejesha Yacouba Songne ambaye yupo kikosini kwa sasa japo hatumiki wala hakutambulishwa kikosi cha sasa.

Inaelezwa awali benchi la ufundi la klabu hiyo lilikuwa lipiga ana..ana…anaa doo, juu ya nani apigwe chini kati ya Lazarous Kambole, Jesus Moloko na Makambo na kura kumwangukia Mzambia.

Inadaiwa kushindwa kuwika katika ligi tangu atue, licha ya kufunga mabao muhimu yaliyoiwezesha Yanga kubeba taji la ASFC, kulifanya makocha kugawanyika juu ya hatma yake, lakini salama ikapatikana kutokana na Kambole kuwa majeruhi wa muda mrefu.

Hata hivyo, inadaiwa Makambo ameelezwa sasa ni lazima apige shoo ya maana kila anapopata nafasi, la sivyo atapishana na Songne dirisha dogo, kwani moto wa Mbukinabe huyo aliyesajiliwa misimu miwili iliyopita akitoka Asante Kotoko ya Ghana ni mkali japo majeraha yalimtibulia na kumweka nje kwa muda mrefu.

Yanga iliamua kumtoa Kambole kwenda Wakiso Giants, ili Kisinda aingie na ataanza kuwasha moto mechi za Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa ataanzia raundi zijazo kutegemeana na matokeo ya juzi usiku, Yanga iliporudiana na Zalan ya Sudan Kusini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here