Baada ya ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Zalan Fc Wananchi wakitinga hatua ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kutakuwa na mapumnziko ya takribani siku 10 kupicha michezo ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya FIFA.
Mchezo utakaofuata ni wa ligi kuu dhidi ya Ihefu FC ambao utapigwa Septemba 29, 2022 mkoani Mbeya.
Pengine huu utakuwa mchezo wa kwanza Mashabiki wa Yanga kumshuhudia Tuisila Kisinda aliyerejea kutoka klabu ya RS Berkane.
Kisinda amepata leseni inayomruhusu kucheza mechi za ligi kuu na kombe la FC wakati akisubiri Yanga itinge hatua ya makundi ligi ya mabingwa/Shirikisho aweze kushiriki michuano hiyo ya CAF.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE