Home KITAIFA KUELEKEA MECHI DHIDI YA WASUDAN, MASTAA WOTE YANGA WAITWA FASTA

KUELEKEA MECHI DHIDI YA WASUDAN, MASTAA WOTE YANGA WAITWA FASTA

0

Wachezaji wa Kikosi cha Yanga, David Bryson na Aboutwalib Mshery waliofanikiwa kusonga hatua inayofuata wakiwa na timu ya taifa ya Tanzania ya U23 tayari wamerejea na wataingia kambini moja kwa moja kuungana na wenzao.

Hawa walikuwa miongoni mwa wachezaji waliohakikisha timu ya taifa ya Tanzania U-23 kutoka sare ya mabao matatu dhidi ya Sudan Kusini na kufanikiwa kutinga hatua inayofuata kutokana na bao la ugenini.

Katika mapumziko haya mafupi, wachezaji saba wa Yanga walijumuishwa kwenye timu zao za taifa ambao ni pamoja na Kibwana Shomari, Dickson Job, Denis Nkane (Taifa Stars), Stefano Aziz (Burkina Faso) na Djigui Diarra (Mali).

Wachezaji wawili wa kimataifa (Diarra na Aziz KI) wanatarajia kuingia nchini leo Septemba 30, 2022 na wale wa Taifa Stars nao wataingia leo kambini.

Aidha, nyota kutoka Uganda, Khalid Aucho anaendelea vizuri na mazoezi baada ya kupata jeraha kidogo hivi karibuni wakati huo huo Feisal Salum nae akiendelea na mazoezi mepesi.

Bernard Morrison tayari ameanza mazoezi na wenzake na yupo timamu kimwili kwa ajili ya michezo ijayo ya Ligi na kimataifa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here