Home KITAIFA KUELEKEA MECHI YA KESHO CAF, MASTAA HAWA YANGA KUKOSEKANA

KUELEKEA MECHI YA KESHO CAF, MASTAA HAWA YANGA KUKOSEKANA

0

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema anatarajia kuwakosa wachezaji wake watatu kwenye mchezo wa kesho Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan.

Yanga watakuwa wenyeji kwenye mchezo huo unaochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wakishuka dimbani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa uwanja huo.

Nabi alisema anatarajia kumkosa Djuma Shaban, Khalid Aucho na Bernard Morrison ambao amesema kuwa waliumia kwenye mechi zilizopita.

“Kukosekana kwao kutatoa nafasi kwa wachezaji wengine kuna Joyce Lomalisa atacheza nafasi ya beki akiziba pengo la Djuma,” alisema na kuongeza;

“Kutakuwa na mabadiliko mengi kwenye kikosi cha kesho lakini sitafanya mabadiliko yatakayoniumiza nahitaji kuwa na kikosi kizuri ambacho kitaisaidia timu kupata matokeo,”

Wakati huohuo alisema ratiba imekuwa changamoto kwao kutokana na wachezaji wake kushindwa kupata muda wa kupumzika wanacheza mechi mfululizo.

“Ni kweli ratiba ilitolewa mapema lakini hilo haliwezi kunizuia mimi kuzungumza hali halisi iliyopo kwa wachezaji wangu,”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here