Home KITAIFA MAJIBU YA KWA NINI KENNEDY JUMA ANAANZA MBELE YA ONYANGO

MAJIBU YA KWA NINI KENNEDY JUMA ANAANZA MBELE YA ONYANGO

0

Uwepo wa Kocha Juma Mgunda ndani ya kikosi cha Simba umekuwa na neema kwa beki wa timu hiyo, Keneddy Juma aliyeanza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Wanamsimbazi hao huku mwenyewe akisema hana hofu yoyote.

Keneddy licha ya kudumu na ubora mkubwa tangu amejiunga Simba SC akitokea Singida United misimu mitatu iliyopita, hakuwa na uhakika wa namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho.

Beki huyo mzawa amekua akitumika kama mchezaji wa akiba endapo Joash Onyango, Pascal Wawa (ameondoka), Henoc Inonga, Erasto Nyoni na Mohammed Ouattara aliyeongezeka msimu huu, wakiwa na changamoto za kiafya lakini Mgunda amemumini na kumpa nafasi kwenye michezo miwili na kufanya vizuri.

“Kila mchezaji anataka kucheza lakini hamuwezi kucheza wote kila siku. kocha ndiye anaamua ampange nani hivyo ukipangwa au kutopangwa unahitaji kuwa mvumilivu kwani tukiwa kwenye timu wote lengo letu ni moja.” amesema Keneddy

Kenedy aliaanza katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Malawi Nyasa Big Bullet, pia alicheza mchezo wa Mzunguuko wanne wa Ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here