Home KITAIFA MAMBO YAWA MAGUMU KWA KAGERE NA SINGIDA YAKE, ISHU NZIMA IKO HIVI

MAMBO YAWA MAGUMU KWA KAGERE NA SINGIDA YAKE, ISHU NZIMA IKO HIVI

0

MEDDIE Kagere ni miongoni mwa nyota walioanza kikosi cha kwanza kilichopangwa na Kocha Mkuu Hans Pluijm mwenye tuzo ya kocha bora kwa mwezi Agosti.


Mchezo huo wa ligi umechezwa Uwanja wa Liti,baada ya dakika 90 ubao umesoma Singinda Big Stars 0-0 Dodoma Jiji.

Mchezo wa jana Dodoma Jiji wamekamilisha wakiwa pungufu baada ya nyota wao Collins Opare kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kuwa alionyeshwa kadi mbili za njano na mwamuzi wa kati Hance Mabena.

Ni kwa mara ya kwanza Singida Big Stars inabanwa mbavu ikiwa Uwanja wa Liti kwa kuwa kwenye mechi mbili za mwanzo iliambulia pointi tatu na kufikisha pointi sita.

Mchezo ulikuwa na matumizi ya nguvu kubwa na kadi za njano zilitolewa kwenye mchezo huo na miongoni mwa walioonyeshwa kadi hizo ni pamoja na Amiss Tambwe wa Singida Big Stars, Hassan Kessy wa Dodoma Jiji.

Masoud Djuma ana kibarua kizito cha kurejesha ubora wa Dodoma Jiji kwa kuwa imeanza msimu wa 2022/23 kwa mwendo wa kusuasua.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here