Home KITAIFA MANARA : WAZUNGU HAWAWEZI KUHANGAIKA NA “MVUNJA KUNI” MWAKINYO….YEYE NI KAMA CHALE...

MANARA : WAZUNGU HAWAWEZI KUHANGAIKA NA “MVUNJA KUNI” MWAKINYO….YEYE NI KAMA CHALE TU..HANA MAAJABU…

0

 

Juzi, Septemba 3, 2022 Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo alipoteza pambano dhidi ya Bondia Muingereza, Liam Smith kwa TKO raundi ya 4 katika pambano lenye raundi 12.

Mwakinyo alianza pambano vizuri na wakati likiendelea alionekana kuumia mguu kiasi cha Muamuzi kusimamisha pambano ambalo kabla ya round ya nne kumalizika Mwakinyo alionekana kapiga goti chini.

Baada ya pambano hilo kumalizika Mwakinyo alijirekodi video fupi ikiomuonesha akiomba radhi kwa Watanzania na kueleza sababu zilizofanya ashindwa kumkabili Muingereza Liam Smith ambapo alisema miongoni mwa vilivyofanya ashindwe pambano hilo ni kukosekana kwa viatu ambavyo alipaswa avae katika pambano hilo huku akidai kuwa begi lililokuwa limebeba viatu hivyo lilipotea Airport wakati akielekea katika pambano hilo.

Sasa mengi yamesemwa na miongoni yaliyoingia katika vichwa vya habari ni baada ya kusambaa kwa sauti inayodaiwa ya Haji Manara ambaye ameponda vibaya Mwakinyo kwa kupoteza pambano hilo akidai kuwa amewalaghai mashabiki na Watanzania.

“Hawa wazungu hawawezi kuhangaika na huyu mvunja kuni, kwanza hawajui kama Nike yao imevaliwa. Huyu muongo muongo wanamdharau, wameona hawawezi kuhangaika na huyu lofa.

“Nike kampuni kubwa, wameona impact yake ni ndogo, wameangalia pambano lake haliwezi kutazamwa na watu hata milioni 50 dunia nzima, Nike wanatazamwa na zaidi ya watu bilioni moja.

“Huyu wamemuona kama chale tu, amefanya uchale basi. Eti vitau vilikuwa ninamfinya ndio akapata enka, sisi sote tumecheza mpira tunabanwa na viatu lakini huwezi kupata enka, uongo wa kizamani huo, afadhari angepata lengelenge, enka na viatu kukubana wapi na wapi? Pumbavu mkubwa, amenitoa mood nimezidi kummindi sana. Watu waongo waongo katika michezo siwapendi, kwa nini unataka kutuongopea?

“Eti umepoteza begi? Kwanza Ulaya mambo ya kupoteza mabegi hayapo. Begi litoke Marekani likapotee Uingereza? Washavuka huko. Hiyo ndege ya kichupli chupli, watu washatoka huko vitu ni digital sasa hivi,” amesema Manara.

THIS POST IS POSTED IN SOKA LEO AND APPEAR IN THIS APP

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here