Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez ametajwa katika orodha kama makamu rais wa Kamati ya CAF ya maandalizi ya mashindano ya vilabu na usimamizi wa mfumo wa Leseni za klabu kuanzia mwaka huu mpaka 2024.
Barbara ni Mwanamke pekee kwenye orodha hiyo chini ya Rais Ahmed Yahya ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Mauritania.
Hatua hiyo ya Mtendaji mkuu huyo wa Simba SC kupata nafasi ya uongozi kwenye moja ya Kamati ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ni hatua nyingine ya Simba SC na Tanzania kwa ujumla kuendelea kuvuka mipaka na kufahamika Kimataifa.