Wekundu wa Msimbazi, Klabu ya Simba SC imeibuka na alama tatu katika mchezo mgumu mbele ya maafande wa Tanzania Prison Jijini Mbeya.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara umepigwa jioni ya jana katika Uwanja wa Sokoine na Simba kuibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0.
Goli pekee la ushindi la Simba limefungwa na Kiungo Jonas Mkude dakika ya 86 akimaliza mpira wa kichwa uliopigwa na Kibu Denis.
Ushindi huo wa Simba unaifanya kusogea kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwa na alama 10 sawa na Yanga huku kila timu ikiwa na magoli 6.
Prison wamejikuta wakimaliza pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuoneshwa kadi nyekundu
Pamoja na kufungwa na Simba, Pia Prisons wamajikuta wakitiliwa mchanga kwenye ‘tongwa’ yao mara baada ya kujikuta wakikosa pia ahadi ya pesa zaidi ya milioni ishirini ambazo walihaidiwa na wadhamini wao wapya endapo wangepata matokeo.
Huku kwa upande wa Simba, ukiwa ni ushinidi muhimu zaidi kwao haswa Kocha Mgunda ambaye huu ni ushindi wake wa pili toka akabidhiwe kukaimu nafasi ya kocha mkuu.