Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane, tangu ahudhurie Wiki ya Mwananchi amekuwa akiizungumzia Yanga mara kwa mara.
Safrai hii ameshare nasi kile kilichomvutia wakati wa wiki ya Wananchi ni namna ya Mashabiki wa Yanga wanavyoendana na mshambuliaji wao Fiston Kalala Mayele pindi anaposhangilia goli.
Pitso kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika (Tafsiri isiyo Rasmi): “Nilipoalikwa kuwa sehemu ya wiki ya Wananchi, nilifanikiwa kushuhudia ule ushangiliaji maarufu! Niamini, uwanja mzima ulisimama na kuiga, uzoefu huo ulibaki kwenye mfumo wangu hadi leo. Heri ya Soka ya Tanzania!
Ujumbe huo unaonesha dhahiri ni kwa namna gani kocha huyo anaifuatilia ligi ya Tanzania hasa klabu ya Yanga.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE