Home KITAIFA MWAKINYO AANZA KUANIKA MAPYA KUHUSU ISHU YA KUPIGWA NA MZUNGU

MWAKINYO AANZA KUANIKA MAPYA KUHUSU ISHU YA KUPIGWA NA MZUNGU

0

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amelizungumzia pambano lake alilopoteza raundi ya 4 kwa TKO dhidi ya Bondia Liam Smith wa Uingereza, Septemba 04, 2022. Mwakinyo amesema ilimuumiza lakini haijamkatisha tamaa.
Mwakinyo amesema pambano lake na Liam Smith lilikuwa na nafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake na kumuondoa katika umasikini.

”Nimekosa hela nyingi sana kutokushinda lile pambano, lakini sijawahi kukata tamaa na silaumu mipango ya Mungu. Ningeweza kuuaga umasikini.

“Ningeweza kukodisha bodaboda wote wa Tanga, kila mmoja ningempa bajaji tano halafu angekuwa ananirudishia hela kwa namna anayotaka mwenyewe,” amesema wakinyo.

Mwakinyo pia ameongeza kwamba endapo angekuwa ameshinda kwenye lile pambano, ilikuwa ni nafasi ya kumsogezea mkataba wa pambano jingine la pesa ndefu zaidi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here