Home KITAIFA MWAKINYO AFUNGUKA ALICHOPEWA KABLA YA PAMBANO KIKAMPONZA….AIKATAA TKO YA SMITH…

MWAKINYO AFUNGUKA ALICHOPEWA KABLA YA PAMBANO KIKAMPONZA….AIKATAA TKO YA SMITH…

0

 

Bondia wa kimataifa kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo ‘Champeez’ amepoteza pambano dhidi ya Liam Smith baada ya kupigwa kwa TKO.

Pambano hilo lililokuwa na mizunguko 12 limeishia mzunguko wa 4 baada ya Mwakinyo kupiga goti wakati pambano likiendelea.

Baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Liam Smith, Bondia Hassan Mwakinyo ameelezea kilichotokea huku akisema yupo tayari kurudiana na mpinzani wake

Amesema alipoteza begi lake alipokuwa Uwanja wa Ndege, hivyo ilibidi Wenyeji wake wampatie viatu vingine ambavyo vilikuwa vinamfinya na kumuumiza Kifundo cha mguu.

Amesema wakati wa pambano alipokuwa anakabiliana na hali hiyo ilibidi ateme ‘MouthGuard’ maana Sheria za Boxing zinasema refa anatakiwa amsimamishe mpinzani na kuuliza nini kinaendelea.

Ameongeza; “Mechi kama mlivyoiona, begi langu lilipotea Airport wakati nakuja huku kwa hiyo Jamaa imebidi wanipe viatu vingine, wakati napigana viatu vyao vilikua vinanifinya sana ndio maana nikatema #mouthguard chini kwa sababu sheria ya boxing ukitema #mouthguard chini manake refa anatakiwa kuiokota amsimamishe mpinzani aniulize kunaendelea nini.

“Aliponiuliza nikamwambia viatu vinanifinya kama nimepqta enka, akaniuluza kama naweza kuendelea nikamjibu ndio. Lakini nilipoendelea muda kidogo vikaanza kuniumiza tena, nikapiga goti, mpinzani akaendelea kunipiga, refa akamaliza pambano papo hapo.

“Mimi sihesabu kama ni TKO kwa sababu nyinyi wenyewe mmeona, tunajaribu kuongea na promota nirudiane naye kwa sababu bado nina uwezo wa kufanya kitu,” amesema Hassan Mwakinyo.

THIS POST IS POSTED IN SOKA LEO AND APPEAR IN THIS APP

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here