VIJANA wapya wa Yanga kazini Ally Kamwe na Privadinyo kwenye idara ya Habari na Mawasiliano wametambulishwa rasmi jana Septemba 27.
Kamwe ni mchambuzi na mwandishi wa Habari za Michezo sawa na ilivyo kwa Privadiny ambao wote ni familia ya waandishi wa Habari.
Pia Haji Mfikirwa yeye atakuwa kwenye kitengo cha fedha wakiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Yanga.
Andrew Mtine ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Yanga naye ametambulishwa jana pia hivyo anaanza kazi na safu mpya kwenye idara ya habari.
Ni Haji Manara yeye bado ni msemaji wa Yanga lakini amekuwa kando kutokana na kufungiwa miaka miwili huku Hassan Bumbuli akiwa hajaongezewa mkataba baada ya kumaliza kandarasi yake Agosti.