Home KITAIFA PAMOJA NA KUFUNGA ‘HAT-TRICK’ JUZI…MAYELE AKOLEZA MSIMAMO WAKE DHIDI YA YANGA KWENYE...

PAMOJA NA KUFUNGA ‘HAT-TRICK’ JUZI…MAYELE AKOLEZA MSIMAMO WAKE DHIDI YA YANGA KWENYE MECHI ZA CAF

0

STRAIKA wa Yanga, Fiston Mayele ameanza kufukuzia moto wa kuvunja ufalme wa lejendi, Mrisho Ngassa ambaye ndiye aliweka rekodi ya kufunga hat-trick kwa timu za Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ngassa alianza kufunga hat-trick ya kwanza Februari 8, 2014 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya Comoro, Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 7-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa, hakuishia hapo akafunga nyingine kwenye mchezo wa marudiano Wanajangwani wakishinda mabao 5-2 ugenini.

Ngassa ambaye alikuwa kwenye kiwango cha juu wakati huo, mchezo mwingine wa CAF alifunga hat trick ya mabao manne, Yanga ikishinda mabao 6-0 dhidi ya Etoile d’or ilikuwa Februari 15, 2016. Imepita miaka sita tangu Ngasa afunge hat -trick ya mwisho 2016, ambapo Mayele amefunga ya kwanza dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini.

Mayele amefunga hat -trick hiyo, Yanga ikishinda mabao 4-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa huku akiweka mpira kwenye tumbo lake na kunyonya kidole kuashiria anatarajia kupata mtoto.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here