Home KITAIFA PAMOJA NA KULAMBA MAISHA YANGA, PRIVA AJIKANA KATU KATU

PAMOJA NA KULAMBA MAISHA YANGA, PRIVA AJIKANA KATU KATU

0

Msimamizi wa Maudhui ya Mitandaoni (Digital Manager) ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Priva Abiudi Shayo amesema nafasi aliyoipata ndani ya klabu hiyo naitazama kama chachu ya kuwahamasisha vijana wa kitanzania kuaminiwa katika taasisi kubwa.

Pviva ‘Privadinho’ alitangazwa kushika nafasi hiyo jana Jumanne (Septemba 27) sambamba na mwenzake Ally Kamwe ambaye anakuwa Afisa Habari wa Young Africans, akirithi nafasi ya Hassan Bumbuli.

Amesema: “Nafasi niliyoipata Young Africans siingalii zaidi kwa upande wangu ila naiangalia kama chachu na hamasa kwa vijana”

“Mimi bado ni kijana mdogo lakini tazama historia na ukubwa klabu ya Young Africans. Ni klabu kubwa si tu Tanzania bali hata nje ya mipaka ya Tanzania.”

“Taasisi kubwa kama Young Africans imeonesha imani vijana wadogo, basi ni hamasa kubwa kwa vijana ambao wanakuja kwenye tasnia iwe ni Waandishi au Wachambuzi, tayari kuna mwanga umeanza kuonekana.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here