Baada ya kurejea kwenye kikosi, Straika wa Azam FC, Idd Nado amesema kuwa mashabiki zake wategemee makubwa zaidi kutoka kwake kwa msimu huu.
Nado alikuwa nje ya kikosi cha Azam kwa muda mrefu hiyo ni baada ya kupata majeraha ya goti ambayo yalimuweka nje kwa miezi kadhaa.
Nyota huyo amefanikiwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya TP Mazembe juzi ijumaa tangu aanze mazoezi na kikosi hicho.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Idd alisema kuwa “Kwanza nimefurahi sana kurejea tena uwanjani na kuwa sehemu ya kikosi.
“Mashabiki wangu nawaahidi wategemee mazuri kutoka kwangu kwa msimu huu kwani mipango yangu ni kufanya vizuri zaidi ya vile nilivyokuwa hapo awali.”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE