Home KITAIFA RASMI MANARA AKIRI KUMWAGANA NA MKEWE WALIYEFUNGA NAYE NDOA KWA MBWEMBWE

RASMI MANARA AKIRI KUMWAGANA NA MKEWE WALIYEFUNGA NAYE NDOA KWA MBWEMBWE

0

Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amekiri kuachana na mke wake wa tatu Naheeda Abdallah ambaye alifunga naye ndoa usiku wa Desemba 10, 2020.

Manara amesema hayo wakati akijibu swali la mtangazaji wa Wasafi Media, Diva The Bawse.

“Nimeachana na mke wangu , sjampa talaka bado nasubiri taratibu za kisheria ila nammiss pia,” amesema Haji Manara.

Ikumbukwe kuwa ndoa hiyo ilivunja rekodi kwa kuhudhuriwa na mastaa na viongozi wakubwa wa siasa na dini nchini na kuvunja rekodi ya mauzo na hakimiliki za maonyesho kununuliwa na Azam TV.

Miezi michache baadaye stori zikaanza kusambaa kuwa ndoa hiyo imevunjika kutokana na migogoro ya kifamilia lakini taarifa hizo hazikuwahi kuthibitishwa na wawili hao ama wanafamilia.

Aidha, mnamo Aprili 14 2022, Manara aliongeza mke wa pili anayefahamika kwa jina la Rubynah Salum na kufunga naye ndoa huku akidai kuwa ana uwezo wa kuongeza mke wa tatu ama wa nne kwani anaweza kuwamudu wote na kuwahudumia.

Kuhusu mwanamke aliyemtambulisha kama msaidizi wake binafsi, Manara amesema; “Watu wanashangaa mimi kuwa na Msaidizi wa kazi zangu mzuri vile, niko nae muda mrefu nasafiri nae kikazi, naweza nikamuoa pia ikiwezekana,” amesema Manara.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here