Home KITAIFA TAIFA STARS YAWAFUATA WAARABU ASUBUHI ASUBUHI

TAIFA STARS YAWAFUATA WAARABU ASUBUHI ASUBUHI

0

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kimeondoka mapema leo Jumanne (Septemba 20) alfajiri kuelekea Libya, tayari kwa Michezo ya Kimataifa ya Kirafiki.

‘Taifa Stats’ itacheza michezo hiyo ya Kimataifa ya Kirafiki katika Kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda na baadae Timu ya Taifa ya Libya.

Taifa Stars itaanza kupapatuana na Uganda Jumamosi (Septemba 24), kisha mchezo wa pili dhidi ya Libya umepangwa kuuguruma Septemba 27.

Michezo hiyo ya Kimataifa ya Kirafiki ni kwa ajili ya kuiandaa Taifa Stars kuelekea Michezo ya Kuwania Kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ zitakazounguruma nchini Ivory Coast.

Katika harakati za kusaka nafasi ya kucheza Fainali za AFCON 2023, Stars itacheza dhidi ya Uganda mwezi Oktoba mjini Kampala, kabla ya kurudiana tena na Wababe hao wa Afrika Mashariki jijini Dar es salaam.

Stars ipo Kundi F sanjari na timu za Taifa za Niger, Algeria na Uganda.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here