Home KITAIFA UKIMYA NA KUTOONEKANA KWAKE UWANJANI..HUU HAPA UKWELI WA HALI HALISI YA DAVID...

UKIMYA NA KUTOONEKANA KWAKE UWANJANI..HUU HAPA UKWELI WA HALI HALISI YA DAVID NKANE NA YANGA YAKE

0

Mchezaji kutoka timu moja kwenda timu nyingine hasa kutoka kwenye timu ya daraja dogo kwenda timu ya daraja la juu ni mafanikio makubwa kwa mchezaji mwenye ndoto kubwa.

Kwenye ligi yetu wachezaji wengi wanaofanya vizuri wakiwa na timu ndogo mara nyingi wanapofanikiwa kupata nafasi ya kuzichezea hizi timu zetu kubwa wengi wao wanashindwa kuendelea kuonyesha ubora wao ambao uliwatoa timu ndogo kuwapeleka timu kubwa.

Sitaki ukumbuke kuhusu kina Adam Salamba,Marcelo Kaheza,Ditram Nchimbi na wengine wengi hawa wote walikuwa na viwango vikubwa sana wakiwa na timu zao lakini baada ya kusajiliwa na timu kubwa walishindwa kuwa na muendelezo mzuri wa kuendelea kufanya vizuri.

Sikia nikuambie kuhusu Denis Nkane kijana aliyekuwa lulu katika timu ya Biashara United kufanya vizuri kwake kukamleta Jangwani na anaendelea kuonyesha kwanini anastahili kuivaa jezi ya Yanga.

Ninachoamini Nkane mpaka sasa hakuna alichopoteza kuwa kwake Yanga ni mahali sahihi sana tangu ameanza kuivaa jezi namba 16 amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye timu licha ya kutopata nafasi ya kucheza mda mwingi.

Chini ya kocha Nabi Nkane amekuwa na improvement kubwa sana kama unaona Nkane siyo yule unatakiwa utambue wachezaji alikuwa na Biashara United ni tofauti na wachezaji aliokutana nao Yanga hata aina ya timu pia kuna mabadiliko makubwa.

Naamini Nkane kadri siku zinavyokwenda atakuwa bora zaidi uwepo wa mwalimu Nabi naona kabisa Nkane anaenda kutuprove wrong wengi wenye fikra hafifu za mchezo wa mpira.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here