Home KITAIFA UNAAMBIWA WALE WAMALAWI KILA WAKIMUOTA CHAMA, WANAPAGAWA NA MECHI YA JPILI

UNAAMBIWA WALE WAMALAWI KILA WAKIMUOTA CHAMA, WANAPAGAWA NA MECHI YA JPILI

0

Kocha Mkuu wa Nyasa Big Bullets, Kalisto Pasuwa ameweka wazi kuwa watakuwa kwenye wakati mgumu zaidi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Simba huku akisisitiza ubora wa wachezaji wa timu hiyo akiwemo Clatous Chama ulivuruga mipango yake.

Pasuwa ametoa kauli hiyo kufuatia matokeo ya mchezo wa kwanza ambao walipoteza kwa kipigo cha mabao 2-0 uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajia kupigwa Septemba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Pasuwa alisema kuwa kipigo walichopokea kutoka kwa wapinzani wao kimewapa ugumu mkubwa wa kuweza kufanikiwa kupata matokeo makubwa katika mchezo wa marudiano kutokana na ubora wa Simba wanapokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

“Kazi yetu imekuwa kubwa na ngumi mara mbili kwa sababu tumekubali kupoteza kwa kuwa tuliwaheshimu sana wakaweza kutuadhibu kwa urahisi lakini ubora wa wachezaji wake umechangia hasa yule mwenye jezi 17 (Chama) alikuwa kikwazo na mwepesi wa kufanya maamuzi aliyowapa faida ya kushinda.

“Natambua safari yetu itakuwa ngumu kwa sababu Simba wanapokuwa nyumbani wanakuwa katika ubora na wakatili lakini bado tunatafuta namna ya kuweza kufikia katika malengo na nia ambayo tumeweza kujiwekea kwa kuhakikisha tunaweza kupambana kupata matokeo kwa kuwa hatuna cha kupoteza zaidi ya kujitoa,” alisema Pasuwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here