Tulishazoea na kuaminishwa kuwa makocha wa kigeni ndio wana uwezo wa kuziongoza timu zetu hasa katika michuano ya kimataifa.
Ingawa inawezekana bado ni mapema, lakini kocha mzawa Juma Mgunda aliyechukuliwa kwa muda, akiwa chini ya usaidizi wa Selemani Matola ameweza kuivusha Simba ( iliyoachana na kocha wake Mserbia Maki Zoran) kwa mafanikio katika mechi zake za hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla ( aggregate) 4-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi.
Katika michuano hii, tunaweza kusema hakuna timu lelemama, ingawa zipo timu zinazoaminika kuwa kubwa zaidi ( vigogo) na zenye uzoefu, maarifa na rasilimali fedha kwa ajili ya ushindani.
Waswahili husema ‘Nyota njema huonekana asubuhi’.
Je, kwa hatua hii ya awali, msomaji wa Soka Leo unampa asilimia ngapi kocha Mgunda kuelekea mechi zijazo za michuano hii mikubwa barani Afrika?