Home KITAIFA WAINGEREZA WAMFUNGIA MWAKINYO KUPIGANA NCHINI KWAO

WAINGEREZA WAMFUNGIA MWAKINYO KUPIGANA NCHINI KWAO

0

Bodi ya ngumi za kulipwa Nchini Uingereza (BBBC) imemfungia Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo kucheza ngumi nchini humo.

Chanzo cha Mwakinyo kufungiwa kucheza nchini humo hakijawekwa wazi lakini imeripotiwa kuwa alitoa maneno ya kuwachafua baada ya pambano lake na Smith.

Hatua hii ya Bondia huyo namba moja Nchini kufungiwa inakuja siku kadhaa tangu alipozichapa na Liam Smith nchini humo na kupigwa kwa TKO katika raundi ya nne.

Hata hivyo Mwakinyo alidai alidai kuwa hakupigwa badala yake alipiga goti kutoa ishara kwa refa wa pambano hilo kuwa hayuko sawa, lakini refa alimaliza pambano.

Mwakinyo aliongeza kuwa sababu ya kupiga goti na kutema mouth guard alitaka kumweleza refa kuwa viatu vinambana anahisi kupata enka na kushindwa kucheza vizuri.

Hii inatokana na kile alichokieleza kuwa begi lenye vifaa vyake vikiwemo viatu vya kuchezwa lilisahaulika Amsterdam Uholanzi wakati akitoka Marekani kwenda Uingereza hivyo akalazimika kupewa viatu vingine na wapinzani wake ambavyo alidai vilimbana na kumnyima comfotability ya kucheza.

Aidha, baadaye Mwakinyo alidai kuwa amezungumza na promota wa pambano hilo na kukubali lirudiwe hapo hapo Liverpool Uingereza mnamo Januari 23, 2023.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here