Home KITAIFA WAKATI BADO YUPO KWENYE KIFUNGO CHA TFF, MORRISON AZIDISHA ‘UGWADU’ YANGA

WAKATI BADO YUPO KWENYE KIFUNGO CHA TFF, MORRISON AZIDISHA ‘UGWADU’ YANGA

0

Kiungo wa Yanga, Bernard Morrison amezidi kuwa imara hali yake na tayari ameanza mazoezi na wachezaji wenzake.

Nyota huyo alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambao waligawana pointi mojamoja.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-2 Azam FC na Morrison aliyeyusha dakika 90 lakini alikuwa amepata maumivu.

Licha ya kuanza mazoezi nyota huyo hatacheza mechi tatu zinazofuata kwenye ligi za Yanga baada ya kufungiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi iliyo chini ya Shirikisho la Mpira Tanzania, (TFF).

Sababu ya nyota huyo mwenye bao moja ndani ya ligi ambalo aliwatungua Coastal Union Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni kile kilichoelezwa kuwa alimkanyanga kwa makusudi mchezaji wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda.

Miongoni mwa mechi ambazo Morrison atazikosa msimu huu ni pamoja na ule dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 23, Uwanja wa Mkapa.

Pia, atawakosa Namungo na Ruvu Shooting kwenye mtiririko wa adhabu hiyo na ametozwa faini ya milioni moja.

Lengo kubwa la Yanga kwa sasa ni kutinga hatua ya Makundi ya Kombe la Mabingwa Afrika ambapo Yanga watacheza mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya mtoano dhidi ya Al Hilal ya Sudan, Oktoba 8, 2022 katika uwanja wa Mkapa.

Licha ya kuwa na wachezaji wengi wazuri lakini Yanga bado wanahitaji uwepo Morrison akiwa timamu kimchezo ili kumtumia na kuhakikisha wanapata matokeo mechi ya nyumbani na ugenini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here