Home KITAIFA WAZAWA SIMBA WANSTAHILI PONGEZI KWA WALICHOKIFANYA

WAZAWA SIMBA WANSTAHILI PONGEZI KWA WALICHOKIFANYA

0

WAZAWA wawili ambao kwa sasa wanakinoa kikosi cha Simba wote wameanza mwendo wao kwa kasi nzuri wanastahili pongezi na kuongza juhudi zaidi katika kutimiza majukumu yao.

Kocha Mkuu, Juma Mgunda ameanza kibarua kwenye nyakati ngumu kwa kuwa timu ilikuwa bado haijaungana na muunganiko wake ulikuwa unatafutwa.

Kuondoka kwa Zoran Maki na mikoba yake kuwa mikononi mwa Mgunda akishirikiana na Matola kuna jambo limeongezeka kwa wazawa hawa.

Michezo mitatu ambayo wamecheza wameshinda mechi zote mbili za kimataifa na moja ile ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Mwendo wao walianza Big Bulets 0-2 Simba na Simba 2-0 Big Bullets kisha ule wa ligi ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Tanzania Prisons 0-1 Simba.

Mpaka sasa Mgunda ni Kocha Mkuu wa muda na msako wa kocha mpya unaendelea.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Simba ameweka wazi kuwa mwendo wa Mgunda sio mbaya kwa kuwa amepata mazuri.

“Mwendo wake sio mbaya, mechi tatu na zote kashinda, lakini mkataa wake upo wazi kabisa yeye ni kocha mkuu wa muda, kukiwa na taarifa nyingine tutaweka kila kitu wazi,”.
Imeandikwa na Dizo Click.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here