Home KITAIFA YANGA YAZINDUA WEBSITE NA APP KWAAJILI YA MASHABIKI

YANGA YAZINDUA WEBSITE NA APP KWAAJILI YA MASHABIKI

0

Siku ya leo Yanga imefanya uzindua Application pamoja na Tovuti ya timu hiyo ambapo imelenga kuwapa urahisi mashabiki wa Yanga pamoja na wanachama kupata taarifa sahihi pamoja na maudhui mbali mbali kuhusiana na timu.

Uzinduzi huo utaenda kutoa urahisi kwa mashabiki wa Yanga katika kujisajili kudijitali na kuwa wanachama wanaofahamika na hiyo ni kupitia Application hiyo rasmi ya Yanga.

Sambamba na uzinduzi huo Yanga pia imezindua mfumo ambao utarahisisha wanachama kupata kadi kwa haraka.

“Kama tulivyowaahidi wanachama kutatua changamoto ya upatikanaji wa kadi kwa haraka, leo tumetangaza mfumo ambao utarahisisha upatikanaji wa kadi hizo ndani ya muda mfupi, na Maulid Kitenge amekuwa Mwanachama wa kwanza kusajiliwa na kupata Kadi yake papo hapo kwenye hafla ya uzinduzi wa App na website yetu” Hersi Said.

Pia Rais wa yanga Eng. Hersi Said amesema kuwa siku ya leo jioni Yanga itatangaza timu ya vijana ambao watakuwepo katika idara ya habari.

Lakini kitendo cha Maulid Kitenge kuonesha Wazi kuwa ni Mwanachama wa Yanga watu Wameanza kuunganisha kuwa ni dhahiri kuwa ndio anafuata kuwa mrithi wa nafasi ya afisa habari wa Yanga.

Huku tetesi kuhusu Ali Kamwe naye zikiwa bado za moto.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here