Home KITAIFA AHMED ALLY AIBUKA NA HOJA MPYA KUELEKEA DABI KESHO KUTWA

AHMED ALLY AIBUKA NA HOJA MPYA KUELEKEA DABI KESHO KUTWA

0

Kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kupigwa Jumapili hii, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa watani zao Yanga wanafahamu ukubwa wa Simba ndiyo maana mara zote huingia kwa kuwakamia katika mchezo dhidi yao, lakini akawachimba mkwara mzito kwa kusema kwa moto walionao sasa basi wajiandae.

Mara baada ya kumaliza ratiba za michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumapili ijayo Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Yanga kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo ya mzunguko wa kwanza itakayopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Timu hizo mbili Juzi Jumapili zilikuwa na vibarua vigumu vya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga walikuwa ugenini dhidi ya Al Hilal ya Sudan, huku Simba wao wakiikaribisha CD Primeiro de Agosto ya Angola.

Ally alisema: “Kwetu mchezo wa Jumapili ijayo ni wa kawaida sana, hatuna presha na tunajua kwa kiasi kikubwa wapinzani wetu wanajua ukubwa wa Simba ndiyo maana mara zote wakikutana na sisi wanatukamia kwa kuwa ubingwa wao ni kutufunga sisi.

“Lakini hatuwezi kuacha kila muda watumie faida ya kutukamia kupata matokeo, kikosi chetu kina kiwango bora kwa sasa na watani wajipange vizuri” alisema Ahmed Ally.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here