Home KITAIFA AHMED ALLY: HATUKUPATA TULICHOTAKA KWA YANGA

AHMED ALLY: HATUKUPATA TULICHOTAKA KWA YANGA

0

KLABU ya Simba imesema haikupata ilichostahili kwenye mechi dhidi ya Yanga, hivyo sasa hasira zao wanazihamishia kwenye mechi dhidi ya Azam FC keshokutwa, Alhamisi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, amesema mioyo ya wanachama na mashabiki wa timu hiyo imekunjamana na hawana furaha hata kidogo kutokana na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga kwenye mechi ambayo waliitawala kwa kiasi kikubwa, hivyo hasira zote zitaelekezwa kwa Azam FC.

“Hatujapata kile ambacho tulikistahili na kukitaka, tunaheshimu matokeo ya ‘dabi’ na mpira wa miguu, lakini hatujapendezwa nayo, ni matokeo ambayo hatukustahili kutokana na ubora wa timu yetu, ukiangalia dakika 90 zote tulikuwa bora sana, lakini mwisho wa siku tumeambulia alama moja, licha ya kwamba ni sare, lakini hatujapendezwa nayo kwa sababu tulistahili zaidi ya hii sare. Niseme tu mpinzani wetu ana bahati kubwa, alistahili kipigo kikubwa sana,” alisema Ahmed.

Alisema kwa sasa nguvu zote zinaelekezwa kwenye mechi dhidi ya Azam FC.

“Anayefuata ni Azam FC, ina kazi kubwa, tuna hasira na sare ya Yanga, mioyo imekunjana, hatuna furaha hata kidogo, timu bora haistahili kupata matokeo hasa kwa mechi ambayo tumeitawala, tunakwenda kukukutana na mpinzani mgumu, lakini tunafahamu wapi pakumshika. Tunajua wameshamfukuza kocha wao, lakini hilo sisi si kazi yetu, kazi yetu ni kuzichukua pointi tatu kwenye mechi hiyo,” alisema.

Ahmed pia aliwapongeza na kuwashukuru mashabiki wao kwa kuwapa sapoti, kuwashangilia muda wote, licha ya ugumu wanaopata.

“Cha kujivunia sisi Simba ni mshabiki wetu walijaa kuliko wenzetu ambao walikuwa wenyeji wa mechi, walikuja na kushangilia muda wote wametuonyesha kuwa hawakati tamaa licha ya kwamba hatukupata ushindi kwenye mechi zilizopita, lakini, wanatupa kinachotahili kutoka kwao, lakini kwa matokeo sisi hatujawapa kile wanachostahili kutoka kwetu,” alisema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here