Home KITAIFA ALI KAMWE ATAMBA KUTOTUMIA ‘VISPIKA’ ILI KUHAMASISHA MASHABIKI, KAMA IFANYAVYO SIMBA

ALI KAMWE ATAMBA KUTOTUMIA ‘VISPIKA’ ILI KUHAMASISHA MASHABIKI, KAMA IFANYAVYO SIMBA

0

Afisa habari Mpya wa Yanga Ali Kamwe ambaye ameianza hivi karibuni kazi yaki klabuni hapo amesema kuwa siku ya Jumatano watakutana na vikundi vyote vya ushangiliaji na kuwakabidhi vitu wanavyohitaji.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa klabu ya Yanga itaita vikundi vyote katika makao makuu ya klabu na kuwakabidhi vifaa vya ushangiliaji kama Bendera pamoja na mafataki.

Kamwe amesema kuwa watavielekeza vikundi namna nzuri ya kushangilia katika mechi yao dhidi ya Al Hilal huku akinadi kuwa Yanga ina wachezaji bora hivyo haiwezi kutumia njia kama anayoitumia Ahmed Ally katika kuhamasisha mashabiki kwa kutumia vispika.

Kamwe pia ameongeza kwa kusema kama siku akionekana anapita mtaani na Vispika akihamasisha mashabiki kuja uwanjani basi ametoa ruhusa ya kuchapwa Bakora.

Ya kwamba Yanga SC ni timu kubwa na imeshavuka zama za kuhamasisha mashabiki na wanachana kufika uwanjani kwa kutumia njia hiyo bali kwa usajili uliofanyika kila mmoja anajua kuwa wachezaji wa Yanga wana ubora hivyo watu watakuja wenyewe kuja kufuata burudani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here