Home KITAIFA ALLY KAMWE: SISI YANGA SC NDIO TUTAAMUA TUFUNGWE LINI TUKITAKA

ALLY KAMWE: SISI YANGA SC NDIO TUTAAMUA TUFUNGWE LINI TUKITAKA

0

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa sasa watapanga wao lini wafungwe ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na uimara walionao.

Kwenye ligi Yanga imecheza mechi 45 bila kufungwa ambapo hivi karibuni walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Simba ambao ni watani zao wa jadi.

Kisha wakacheza na KMC na kupata ushindi wa bao 1-0 kabla ya juzi kuifunga Geita Gold kwa bao 1-0.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hawana mpango wa kupoteza mechi za ligi kwa sasa kutokana na uimara walionao.

“Tumecheza mechi nyingi tangu msimu uliopita bila kufungwa na tunazidi kuendelea kuwa imara kwenye mechi ambazo tunacheza zitafika mpaka 44, 45,47 mpaka sisi labda tuamue kwamba tutafungwa lini.

“Kikubwa ni kuona kwamba mashabiki wanapata furaha na wachezaji wanajua kwamba majukumu yao lazima yatimizwe kwa wao kupata ushindi ndani ya ligi,” amesema Kamwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here