Home KIMATAIFA ANFIELD LIVERPOOL WAGAWANA POINT NA BRIGHTON

ANFIELD LIVERPOOL WAGAWANA POINT NA BRIGHTON

0

VIJANA wa Brighton wameupiga mwingi kweli, wakiwa Uwanja wa Anfield kwa kuwapa tau Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Dakika 90 ubao ulisoma Liverpool 3-3 Brighton huku nyota Leondro Trossard akitupia mabao matatu kwenye mchezo huo.

Alianza dakika ya 4 mapema kabisa kisha akaongeza msumari wa pili dakika ya 17 na 83 ikiwa ni siku nzuri kazini kwa staa huyo wa Brighton.

Mabao ya Roberto Firmino alitupia mawili dakika ya 33, 54 na moja lilikuwa lakujifunga Adam Webster dakika 63.

Sare hiyo inawafanya Liverpool wafikishe pointi 10 na Brighton wakiwa nafasi ya 4 pointi 14 wote wamecheza mechi 7.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here