Home KIMATAIFA ARSENAL YA MOTO YAICHAPA SPURS 3-1

ARSENAL YA MOTO YAICHAPA SPURS 3-1

0

LONDON is red unaambiwa baada ya Arsenal kushinda mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Spurs.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Emirates ulikuwa ni wa ushindani mwanzo mwisho kwa timu zote kusaka ushindi.

Bao la ufunguzi kwa Arsenal lilifungwa na Thomas Partey dakika ya 20 liliwekwa usawa na staa wa Spurs, Harry Kane dakika ya 31 kwa mkwaju wa penalti.

Gabriel Jesus alipachika bao la pili dakika ya 49 na msumari wa tatu ni mali ya Granit Xhaka dakika ya 67.
Spurs ilikamilisha dakika 90 ikiwa pungufu baada ya staa wao Emerson Royal kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 62.

Sasa Arsenal ipo namba moja ikiwa na pointi 21 huku Spurs nafasi ya tatu na pointi 17 zote zimecheza mechi 8.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here