Home KIMATAIFA AZAM FC KAMILI LYBIA, WANATAKA USHINDI

AZAM FC KAMILI LYBIA, WANATAKA USHINDI

0

MATAJIRI wa Dar Azam FC leo watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika raundi ya Pili dhidi ya Al Akhdar ya Libya.

Jana wachezaji hao walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kuanza kuzikimbiza dakika 90 wakiwa ugenini.

Ni nyota 25 wapo nchini Libya miongoni mwao ni pamoja na Prince Dube, Sospeter Bajana na Tepsi Evance chini ya Kocha Mkuu, Denis Lavagne raia wa Ufaransa.

Nyota saba ikiwa ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Keneth Muguna wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo kwa kuwa wamebaki Bongo.

Mfaransa huyo amebainisha kuwa makosa ambayo waliyafanya kwenye mechi zilizopita yanawapa nguvu ya kusaka ushindi kwenye mechi zao.

“Ambacho tunahitaji ni ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza, wachezaji wamekuwa wanafanya kazi kubwa na wanaonyesha kuelewa pale tunapokuwa mazoezini na ikifika kwenye mchezo tunahitaji ushindi.

“Kwenye mechi zilizopita tuliona kuna makosa kwenye kutengeneza nafasi na kuzitumia hivyo kwa mechi zetu nyingine tutajitahidi kutumia nafasi kushinda,” .

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here