Home KITAIFA AZAM FC WAJA NA KAMPENI YA INAWEZEKANA

AZAM FC WAJA NA KAMPENI YA INAWEZEKANA

0

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Azam FC baada ya kete yao ya kwanza kupoteza ugenini wanatarajiwa kurejea leo kuanza kujipanga upya.


Juzi Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Mfaransa Denis Lavagne ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Martrys of February ukisoma Al Akhadar 3-0 Azam FC nchini Libya.


Azam FC ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Dar wikiendi ijayo.


Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa wanarejea kwa ajili ya kufanya maandalizi kuelekea mchezo ujao.


“Tunashukuru mchezo umemalizika salama tunatarajia kurudi kesho, (leo) kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mechi yetu ijayo,” alisema Amin.


Kikosi hicho kimekuja na sera mpya inayokweda kwa jina la Inawezekna wakiwa na imani ya kupata matokeo kwenye mchezo wao wa marudio.


Ni Oktoba 16,2022 Uwanja wa Mkapa mchezo huo wa marudio unatarajiwa kuchezwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here