Home KITAIFA AZAM MAJI KUPWA MAJI KUJAA

AZAM MAJI KUPWA MAJI KUJAA

0

Kabla msimu huu kuanza kipindi kile cha usajili kwa aina ya wachezaji ambao walikuwa wanatua pale Chamazi mashabiki wengi wa soka waliamini Azam FC atakwenda kuwatingisha wakubwa wa Kariakoo.

Bado aina ya wachezaji waliosajiliwa wameshindwa kutoa kile kilicho bora kama slogam yao inavyosema timu bora,bidhaa bora.Kocha AbdiHamid Moalin alimaliza vizuri na ila msimu huu mambo yakawa magumu wakamtimua.

Mfaransa Dennis Lavagne amekuwa hana kikosi cha kwanza ambacho kinacheza angalau mechi tatu au nne wachezaji wanakuwa hao hao. Mabadiliko kila mechi yanajitokeza. Kama huyu kocha ataendelea na matokeo aina hii basi atakuwa hana maisha marefu pale Chamazi.

Namna walivyocheza kwa kujitoa na ari dhidi ya Al Akhdar,ile ari wangehamishia katika mechi za ligi kuu basi wangekuwa wanapata matokeo chanya kila uchwao.

Hadi sasa wamecheza saba za Ligi Kuu,wameshinda mechi tatu,wamefungwa mechi mbili huku wakitoka sare mechi 2. Kwa aina ya usajili waliofanya wangekuwa wanakimbizana na wakubwa wa Kariakoo pale juu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here