Home KITAIFA BAADA YA MASHABIKI KUMSIMANGA SAANA…KIBU DENIS AIBUKA NA KUANIKA ‘UCHAWI’ WAKE SIMBA

BAADA YA MASHABIKI KUMSIMANGA SAANA…KIBU DENIS AIBUKA NA KUANIKA ‘UCHAWI’ WAKE SIMBA

0

Kibu Denis tangu amejiunga na Simba msimu uliopita akitokea Mbeya City amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaopata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza chini ya makocha tofauti waliopita pale Msimbazi na leo amefichua kitu kinachombeba.

Kibu alijiunga na Simba, ikiwa chini na kocha Mfaransa Didier Gomes aliyemuamini na kumpa nafasi na baadaye Gomes aliondoka na timu kuwa chini ya Mnyarwanda Thiery Hitimana ambaye pia alikuwa anampanga Kibu kikosi cha kwanza licha kocha huyo kudumu kikosini hapo kwa muda mfupi.

Baadaye alikuja Mhispaniola, Pablo Franco ambaye alimtumia Kibu kama winga kabla ya kuondoka na kuja Zoran Maki msimu huu ambaye licha ya kukaa muda mfupi alikuwa akimtumia na sasa chini ya Juma Mgunda hali imeendelea kuwa hivyo.

Akizungumza Kibu ameweka wazi kuwa siri kubwa ni kukubali kujifunza kila siku, kujituma na kuwa na nidhamu ya hali ya juu.

“Kuna sababu nyingi zinanifanya niendeleee kuaminika lakini kubwa zaidi nadhani ni hali ya kutochoka kupambana, kujifunza na nidhamu.

“Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wengi bora hivyo hauwezi kupata namba kirahisi kama sio mpambanaji, kuna wakati unatakiwa kukubali kuwa chini na kujifunza kutoka kwa wenzako namna gani unatakiwa kucheza na kuishi nao,” alisema Kibu aliyewahi kuzichezea Kumuyange na Geita Gold na kuongeza;

“Kila mwalimu anakuja na falsafa na mbinu zake, ni ngumu kufiti kote kama utakuwa mjuaji lakini ukituliza akili na kufuata kile anachotaka ufanye na kukifanyia mazoezi ya kutosha, utafanikiwa.” Kuhusu maandalizi ya Simba kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho dhidi ya Primeiro de Agosto ya Angola alisema: “Kama timu tumejipanga kushinda.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here