Home KITAIFA BARUA FUPI KUTOKA KWA IBENGE KWENDA KWA YANGA

BARUA FUPI KUTOKA KWA IBENGE KWENDA KWA YANGA

0

CCL 2022,
KHARTOOM, SUDAN
17 Oktoba 22

Kwa: Wananchi

Asanteni sana kwa kuja kama mlikuwa mnawaza kupindua meza, basi mngeanza kuipundia kule seburlleni kwenu. Hata makundi yalishtushwa sana na ile taarifa ya kondoo aliyepotea miaka 24 katikati ya jua na mvua anataka kurudi kundini.

Nadhani mmefurahia hii radha ya Al Hilal kuliko Al Kasus huku Sudan, kama ikiwezekana jazba na hasira zenu nendeni mkazimalize kwa Simba mwekundu ila jana mlicheza na Simba dume mwenye rangi ya bluu.

Wapendwa Wananchi hayo makundi sio kila mtu anaweza kuingia,maji na mafuta yameanza kujitenga hamna namna “Calm down support Al Hilal” nipeni Morrison na Feitoto nikashinde klabu bingwa.

Kabla sijamaliza nina ujumbe wenu kutoka kwa yule Mwamedi mwenye rasta amewamiss sana,hongereni kwa mchezo mzuri na kila la kheri huko muendako.Mpaka muda mwingine tena karibuni sana Khartoom.

Ni mimi Florent Ibenge wa Kinshasa.

F. Ibenge
Frolent Ibenge
(Mwananchi)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here