Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema amefanikiwa kushinda tuzo ya Balllon d’Or ikiwa ndio mara ya kwanza kwake toka aanze kucheza football.
Mchezaji huyo mwenye miaka 44 msimu uliopita alifanya vizuri akiwa na Real Madrid na kufunga magoli 44 katika mechi 46 alizocheza.
Alifanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya pamoja na taji la Uhispania na Super Cup.
Katika kugombania tuzo hiyo, Benzema alikuwa anashindana dhidi ya wachezaji wengine akiwemo Msenegali Sadio Mane.
Matokeo ya ni kama ifuatavyo.
- Karim Benzema
- Sadio Mané
- Kevin De Bruyne
- Robert Lewandowski
- Mohamed Salah
- Kylian Mbappé
Mwaka uliopita Karim Benzema alimaliza katika nafasi ya nne kwenye tuzo za Ballon d’Or nyuma ya Lionel Messi, Robert Lewandowski na Jorginho.
Hii ni tuzo yake ya kwanza Benzema kushinda.
” Nimejisikia furaha sana kushinda tuzo hii, kiukweli nilifanya jitihada sana,” amesema Benzema.
Sherehe za tuzo hizo zimefanyika usiku wa leo Oktoba 17, 2022 katika jiji la Paris katika Ukumbi wa Théâtre du Châtelet.
Hizi ni tuzo za 66 tangu zianze kutolewa mwaka 1956.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE