Home KIMATAIFA BRIGHTON YAICHAPA CHELSEA 4G

BRIGHTON YAICHAPA CHELSEA 4G

0

UWANJA wa Falmer Brighton wamebaki na pointi tatu zote mazima kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Chelsea mchezo wa Ligi Kuu England.

Bao la ufunguzi lilijazwa kimiani na Leandro Trossad dakika ya 5, Ruben Loftur-cheek alijifunga dakika ya 14 na Trevoh Chabobah alijifunga dakika ya 42 na kufanya mapumziko Brighton kuwa wanaongoza.

Kipindi cha pili bao la Kai Havertz dakika ya 48 liliwaongezea hasira wapinzani wao ambao walifunga bao la nne dakika ya 90 kupitia kwa Pascal Grob.

Kwenye mchezo huo ni mashuti 19 yalipigwa na Brighton kuelekea langoni ambapo ni 9 yalilenga lango huku Chelsea wakipiga mashuti 15 na 7 yalilenga lango.

Kwenye msimamo Brighton wanafikisha pointi 18 wakiwa nafasi ya 8 huku Chelsea wakibaki na pointi 21 nafasi ya tano.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here